Microsoft word - octoba hoja-tovuti

MAJIBU YA HOJA ZA WADAU MBALIMBALI
KWA MWEZI SEPTEMBA NA OCTOBA, 2013.
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwashukuru wadau wote waliotuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa njia ya simu, barua pepe na fecebook page kwa kipindi chote cha mwezi Septemba na Octoba, 2013. Pia tunapenda kuwajulisha wale wote waliotuandikia maoni na maswali wafungue baruapepe zao kwani tumejibu kila swali na kuwatumia katika anwani husika, na baadae kuyaunganisha maswali na maoni yanayofanana na kuyatolea majibu ya jumla kwa faida ya wasomaji wetu wengine ili kuendelea kuelimishana kuhusu masuala yanayohusu utekelezaji wa mchakato wa ajira Serikalini. Swali la 1
BARUA YA WAZI KWA TUME YA AJIRA TANZANIA Mimi Tangia mwaka 2011 ilipo hitimu elimu ya Juu Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) Degree ya Maendeleo ya Mipango ya Fedha na Uwekezaji (Bachelor Degree in Development Finance and Investment Planning),Nimetuma sana Maombi ya kazi kila zinapotangazwa na serikali kupitia Tume ya ajira Tanzania SIJAWAHI KUITWA HATA SIKU MOJA KWENYE USAILI.Kulikoni au hizo ajira mnapeana kwa kujuana,au sisi wengine sio watanzania/hatuna haki,au hatuna dhamana ya kupata ajira.MPAKA SASANIMETUMIA SHILINGI 80,000/= za kutuma barua ya maombi ya kazi kupitia Tume ya ajira Tanzania. Jamii ninaishi nayo kijijini wananishangaa na wanaona kusoma hakuna Maana.Mbaya zaidi Ukoo wetu mimi ndiyo mtu wakwanza kusoma na nimesoma kwataabu sana.NAOMBA MNISAIDIE NINI TAZITO NA NINI KIFANYIKE, ELIMU NIYOIPATA HAINA MAANA, HADI NAJUTA KUGHARAMIA MASOMO YANGU DUH.! Asante tumepokea barua yako, Kwanza nikupe pole kwa hilo lakini fursa bado unayo, Ninachoweza kukujibu ni kwamba inawezekana umetuma maombi mengi kila kazi zinapotangazwa kama unavyoeleza lakini ukawa unatuma maombi kwa kazi ambayo haiendani na taaluma yako uliyosomea kama ambavyo baadhi ya waombaji kazi wanafanya, kwa mfano utakuta kada iliyotangazwa ni Mhasibu daraja la kwanza au Fundi Sanifu Ujenzi halafu wewe ukaomba, utakubaliana nami kwamba hapo huwezi kuitwa kwenye usaili. Suala la msingi kabla ya kutuma maombi yako soma tangazo husika kwa umakini ili kujua sifa za kazi husika. Jambo unalozungumzia la ajira kwa kukujuana huo ni mtazamo hasi ambao hupaswi kuwa nao kwa sababu mchakato huu wa ajira ni wa wazi na hauna upendeleo wa aina yeyoye na unaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya Sera, sheria,kanuni na taratibu zilizounda chombo hiki katika kuwasaidia watanzania kupata kazi kwenye Utumishi wa Umma. Swali la 2
MIMI NI MIONGONI MWA WATU AMBAO WANATAKIWA KURIPOTI KAZINI KATIKA TANGAZO LA KURIPOTI KAZINI LA TAREHE 4.10.2013 SAMAHANI NAOMBA KUPEWA BARUA YA AJIRA ILI NIWEZE KURIPOTI MAPEMA KWA SABABU MAZINGIRA NINAYOISHI KUNIFIKIA BARUA KWA NJIA YA POSTA ITACHELEWA SANA NAOMBA MNITUMIE BARUA HIYO KWA EMAIL HII HAPO JINA LANGU NI MANENO IDDY NGUVA KATIKA FANI YA HAIDROLOJIA FUNDI SANIFU II MAJI EMAIL YANGU NI [email protected] hii itanifikia mapema SAMAHANI KWA USUMBUFU. Asante kwa Ombi lako, Kwanza tunakupa hongera kwa kufaulu na kupangiwa kutuo cha kazi, Sekretarieti ya Ajira inatumia utaratibu wa kutuma barua za waliopangiwa vituo vya kazi kwa kutumia anuani za waombaji walizonyesha katika barua zao za maombi na si vinginevyo. Aidha kwa sababu uliyoitoa kwamba sehemu unayoishi huwezi kupata barua kwa njia ya posta, unaweza kufika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira ili kuangalia uwezekano wa kukupatia nakala ya barua yako ili kukuwezesha kuripoti kutuo cha kazi ulichopangiwa. Mimi nilikuwa mtumishi wa Umma katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini kama Afisa Ugavi, niliamua kuacha kazi baada ya kutoelewana na Mkurugenzi wangu katika mambo mengi, kama vile kunikatalia kwenda kufanya masomo yangu yaani Masters, kwa sasa nimemaliza ingawa nipo katika dissertation. Swali langu ni kwamba ninatamani sana kurudi katika utumishi wa umma hasa katika halmashauri yoyote hasa baada ya kugundua kuwa Halmashauri nyingi sana hazina watumishi wa kutosha wa kada yangu, je inawezekana? na kama inawezekana nifanye utaratibu gani ili nirudi? Nashukuru sana kwa kazi nzuri mnayofanya maana inaonekana Tunashukuru kwa swali lako, upo utaratibu unaotumika kwa watumishi wa Umma kujiendeleza wanapokuwa kazini, aidha kwa suala lako ni tofauti kidogo kwa kuwa uliamua kuacha kazi kwa ajili ya kwenda kusoma bila ruhusa ya mwajiri wako. Kwa mujibu wa maelezo yako bado unatamani kufanya kazi katika utumishi wa Umma tunachoweza kukushauri kufanya ni kuwasilisha maombi yako kwa katibu mkuu utumishi kuelezea hali hiyo yeye ndio mwenye mamlaka ya kukuruhusu kuomba tena kazi katika Utumishi wa Umma baada ya kumuelezea sababu zilizokufanya kuacha kazi. "KUKATISHWA/KUSITISHWA" KWA AJIRA NAOT - DSM Ningependa kupata maelezo ya ufafanuzi juu ya sakata lililomtokea mke wangu aliyekuwa amepangiwa kufanya kazi ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali-ofisi ya Dar es salaam. Mke wangu ana stashahada ya "LOGISTICS & TRANSPORT MANAGEMENT" kutoka Chuo cha Taifa cha usafirishaji alipohitimu na kutunukiwa cheti cha Ordinary Diploma mwaka 2009. Kati ya mwaka 2010 -2011 alifanyiwa usaili wa nafasi ya afisa usafirishaji, usaili ambao ulifanyikia katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (Tanzania Institute of Accountancy-TIA DSM Campus). Baada ya kupita muda mrefu tangu alipofanyiwa usaili hatimaye mwaka jana 2012 mwezi wa nne alipokea barua kutoka kwenu ikimuarifu kuwa amepangiwa kazi ya afisa usafirishaji daraja II katika ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (NAOT) Head office-Dar es salaam, na hivyo barua hiyo ilimtaka aripoti mara moja NAOT, naye akafanya hivyo. Baada ya kuripoti NAOT na kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka kwenu (PSRS) alipokelewa na kupangiwa tarehe ya kuripoti (mwezi wa tano) kwa ajili ya induction ambayo ilifanyika katika hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko Dar es salaam kwa takribani wiki mbili hivi au tatu. Wakati wakiwa huko hotelini wakifanyiwa induction pia walikuwa walijaza baadhi ya documents za taarifa zao binafsi na familia zao ambazo ni za kuwarasimisha katika ajira zao. (Walikuwepo waajiriwa wa nafasi nyengine pia katika induction hiyo). Baada ya kumaliza induction na kurudi ofisini ndipo kizaa zaa kilipoibuka baada ya kufahamishwa na "administration manager" kwamba kukikuwa na jambo la kuweka sawa kwanza kabla ya kuendelea na ajira yake na hivyo kutakiwa arudi nyumbani kwanza asubiri taarifa ya hatma ya ajira yake baada ya muda si mrefu. Alirudi nyumbani akiwa amesononeka sana na akaendelea kusubiri bila majibu na hivyo nikamshauri arudi tena NAO kuulizia hatma ya ajira yake. Niukamshauri awasiliane nanyi na akawaeleza hali hiyo na sekretarieti ikamuahidi kulifuatilia suala hilo na kumpa matumaini kwamba NAOT office mahitaji yao yalikuwa ya mtu mwenye sifa kama zake kwahiyo asiwe na wasiwasi kwakuwa NAOT watakapowasiliana nanyi mngewafahamisha juu ya hilo na kampa matumaini ya kwamba ajira yake haiko shakani hata kidogo. Baada ya kuona muda unakwenda bila kupata updates yoyote ndipo aliamua kwenda kuulizia na akapewa taarifa kuwa NAOT wamebadilisha mahitaji/sifa za afisa usafirishaji wanayemtaka badala ya mtu mwenye stashahada sasa wanataka mtu mwenye stashahada ya juu (Advanced Diploma) kwahiyo asingeweza tena kuendelea na ajira hapo NAOT. Baada ya majibu hayo nilimshauri arudi kwenu kwa ajili ya ushauri zaidi. Kwakweli jibu hilo lilimuumiza sana hadi akajikuta anapata tatizo la pressure kushuka, jambo ambalo lilinigharimu kumhudumia na kumtafutia matibabu. Baada ya taarifa hizo za NAOT alirudi tena kwenu kwa ajili ya kuwajuza kilichomtokea na kutafuta ushauri namsaada kwenu kama mlivyokuwa mmemuahidi lakini kinyume na matarajio yake hakupata msaada alioutarajia na matokeo yake akapoteza nafasi ile ya ajira lakini kibaya zaidi akajikuta anapata madhara ya kiafya ambayo hakuwahi kuwa nayo hapo kabla. Pamoja na ahadi yenu kuwa nafasi nyengine itakapopatikana atapewa kipaumbele lakini tangu wakati huo, mwezi wa tano/sita mwaka 2012 hadi leo hii ninapoandika email hii hajawahi kupata taarifa yoyote kutoka kwenu juu ya hatma ya ajira yake, na jambo hilo limekuwa likimuumiza sana kichwa na kwakweli bila kuweka unafiki mimi na mke wangu tunaamini kwamba ajira yake ilifanyiwa mizengwe NAOT kwa sababu za maslahi binafsi ya uongozi wa NAOT kwasababu hatuamini kwamba hawakujua mtu wanayemuhitaji ni mwenye sifa na vigezo gani wakati wanaleta kwenu ombi la kutafutiw/kupatiwa afisa usafirishaji kama ambavyo waliomba watumishi wa kada nyingine. Kwakuwa sasa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu ajira ya mke wangu ilipoota mbawa na kwakuwa jambo hilo limemletea madhara kiafya na kwakuwa jambo hilo limemfanya akate tamaa kabisa ya kufanya kazi katika utumishi wa umma kitu ambacho kimekuwa ni matamanio yake tangu akiwa anasoma akilenga kuutumikia umma wa watanzania, basi ningependa kutumia nafasi hii kuwafikishia kilio chake na pengine muweze kunisaidia kutushauri nini cha kufanya kwasababu pamoja na kutumia gharama kubwa sana kumsomesha mke wangu lakini sasa amekata tamaa ya kuitumia taaluma yake kwa manufaa ya nchi na yeye mwenyewe binafsi kama alivyotarajia. Naomba kwa leo niishie hapa nikitaraji ya kwamba nitapata maelezo ya majibu yatakayoondoa mashaka yangu pamoja na mke wangu juu ya sakata hilo lililomkuta ambalo kwakweli limetuletea madhara fulani kama familia. Bado nina imani kubwa na taasisi yenu (PSRS) kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ambayo inawawezesha watoto na vijana wa kitanzania toka familia zenye background tofauti na hasa sisi tunaotoka katika familia duni za wakulima wa jembe la mkono ambao wazee wetu wanahangaika kutusomesha kwa shida sana japo kwa kiwango hiki kidogo ili walau tuweze kujimudu kimaisha japo kujipatia mkate wetu wa kila siku kwa njia zilizo halali kabisa na kubwa zaidi kuitumikia nchi yetu. JINA LA MHUSIKA (MKE WANGU); PENDO KIBUNJE MPOCHOLWA-ELIMU YAKE: DIPLOMA IN LOGISTIC & TRANSPORT MANAGEMENT Nawatakia kazi njema sana na naomba kupata majibu yenu kupitia njia hii hii ya email, ama mkitaka mazungumzo zaidi basi mnaweza kunipata kwa njia ya simu yangu ya mkononi ambayo ni 0717053625 Tunashukuru kwa swali lako la kutaka kupewa ufafanuzi, Kwanza nikupe pole kwa usumbufu ulioupata wewe na mkeo kwa namna moja ama nyingine. Kwa mujibu wa maelezo yako baada ya kufuatilia suala lako tulibaini kuwa wakati ambapo usaili unafanyika wakati huo kulikuwa na mchakato wa mabadiliko ya muundo wa utumishi wa Umma katika kada mbalimbali. Katika muundo huo nikitolea mfano wa kada yako ya Afisa Usafirishaji mwombaji/mwajiriwa anapaswa kuwa na stashahada ya juu (Advanced Diploma) au Shahada ya fani hiyo, bila shaka utakubali kwamba mabadiliko hayo ndiyo yaliyokuathiri wewe pamoja na wengine kwa wakati huo na inawezekana NAOT pamoja na kwamba walikwishafanya taratibu za mwanzo za ajira yako walikuwa sahihi kwa kuwa muundo huo ulitoka wakati huo na kuelekeza hivyo na kuanzia wakati huo muundo huo ulianza kutumika rasmi na ndio unaofuatwa kwa kada zote hadi sasa. Aidha Sekretarieti ya Ajira ilikuwa sahihi kukushauri kusubiri kama ingetokea nafasi nyingine inayohitaji mtu mwenye sifa kama ya kwako ili kupangiwa tena kituo cha kazi, kwa bahati mbaya fursa hiyo haikujitokeza hadi sasa kutokana na mabadiliko ya muundo huo katika Utumishi wa Umma. Kutokana na mabadiliko hayo tunachoweza kukushauri ni kujiendeleza katika taaluma yako kwa kiwango cha stashahada ya juu ili uweze kuwa na fursa kubwa zaidi wakati nafasi zitakapokuwa zikijitokeza wakati mwingine. Swali la 5.
Kwanza napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuendesha mchakato wa ajira katika taasisi za serikali na serikali kwa ujumla; lakini naomba kujua jambo moja kutoka kwenu kama nilivyosema hapo juu katika kichwa cha habari, ikitokea mtu ana taaluma zaidi ya moja mfano,ana taaluma ya MOTOR VEHICLE MECHANICS kwa level ya cheti na akawa na SHAHADA YA SHERIA na taasisi ya serikali ikatangaza kazi katika taaluma ya cheti yaani (Motor Vehicle Mechanics) na huyo mtu akapata, je akiwa ndani ya hiyo ajira anaweza kutumia vyeti vyake vya shahada ya taaluma ya sheria kama (re-categorization) au ndio taaluma yake ya shahada itakuwa imefia hapo? pili anaruhusiwa kuomba kazi ndani ya hiyo taasisi au taasisi nyingine ya serikali kwa kutumia shahada ya sheria? nategemea ufafanuzi kutoka kwenu.! Tunapokea pongezi zako, Tunatambua kuwa kuna watu wana taaluma zaidi ya moja kama ulivyoeleza lakini inapotangazwa kazi katika utumishi wa umma mwombaji anapaswa kuzingatia sifa za msingi zilizoainishwa katika kazi husika. Kwa mfano kama kazi iliyotangazwa ni ya Motor Vehicle Mechanics mtu mwenye sifa za kazi hiyo ndiye atakayeomba kulingana na vigezo vya tangazo. Pili kama mtu huyohuyo akiwa kazini na akawa na taaluma ya ziada inapotokea kazi nyingine na ana sifa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na pale ambapo mwajiri anapoona inafaa anaweza kukufanyia Re-categorization kwa mujibu wa vigezo vya kazi husika. Pili, unaruhusiwa kuomba kazi katika taasisi nyingine za umma endapo
kazi imetangazwa na ukawa unakidhi vigezo vya kazi hiyo lakini maelekezo
yake ni kwamba unatakiwa kuzingatia masharti yaliyoko katika Waraka wa
Utumishi wa Umma Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba
2010,
ambao pamoja na mambo mengine unamtaka mwombaji ambae
tayari ni mtumishi wa umma kupitisha barua yake ya maombi ya kazi kwa
mwajiri wake.
Swali la 6.
Poleni kwa kazi- Naomba kuuliza mbona hamkuwahi kutoa majina ya waliofailu usaili wa TIC kwa nafasi ya Manager Foreign Investment iliyofanyika mwezi wa 4 mwaka huu, ni karibu miezi 6 sasa je kuna tatizo gani? Kazi njema Asante kwa swali lako, utakubaliana nami kuwa hiyo ni nafasi kubwa kiutendaji hivyo hata mchakato wake wa ajira unahitaji umakini mkubwa na wakati mwingine unaweza kuchukua muda mrefu kidogo. Kwa mfano kwa
nafasi nyingine za maafisa na kada za chini baada ya usaili kukamilika
majibu ya wanaoitwa kazini hutolewa na Sekretarieti baada ya wiki tatu(3)
lakini nafasi za watendaji wakuu, mameneja, wakurugenzi na nyingine
zinazofanana na hizo mchakato wake unaweza kuchukua muda mrefu
kukamilika kutokana na taratibu za ziada za kushughulikia ikiwemo
upekuzi ambao hufanywa na mamlaka mbalimbali.
Swali la 7.
Habari za majukumu yenu, Mbona kuna kada zingine tulituma maombi tarehe hizo za mwezi watano/sita lakini siioni majina wa wanaoitwa kwenye usaili? Au wao bado? mfano: Forestry Training Institute na MWEKA. Naomba ufafanuzi tafadhari ili nafsi yangu isuuzike! Asante kwa Swali lako, Ni kweli zipo baadhi ya kada ambazo waombaji wake bado hawajaitwa kwenye usaili. Sekretarieti ya Ajira imekuwa ikitoa matangazo ya kazi mara kwa mara na vilevile uendeshaji wa mchakato wa usaili hufanyika kwa awamu kwa kuzingatia uwezo wa kibajeti wa kuendesha usaili na wingi wa waombaji wa kazi. Hivyo tunakushauri kuvuta subra na mara taratibu za uchambuzi wa maombi kukamilika mtajulishwa tarehe rasmi ya usaili. Swali la 8.
Naulizia majina ya tulioomba maafisa lishe kupitia wizara ya afya. Mimi ni afisa lishe niliyemaliza degree chuo kikuu cha sokoine - morogoro. wizara ya afya ilitoa ajira katika kada mbalimbali mwezi april mwaka huu, ikiwemo na maafisa lishe ( nutritionist). tarehe 22 may mwaka huu walitoa tangazo kwa umma kuwa tutachaguliwa na sekretarieti ya ajira ofisi ya raisi. Sasa nimepitia wavuti yenu sijaona kuhusu hayo majina ya maafisa lishe. nauliza kulikoni? Ni kweli ajira hizo zilitangazwa kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii lakini badae zilisitishwa na kutangazwa kuwa mchakato huo utaendeshwa na Sekretarieti ya Ajira. Nafasi hizo zilikuwa ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali zikiwemo halmashauri za Wilaya. Kwa mujibu wa taratibu zilizopo kada ya Maafisa ustawi wa jamii vibali vyake hutolewa kwa kila mwajiri badala ya kupatiwa mwajiri mmoja. Kutokana na kukosewa kwa utaratibu nafasi hizi zilifutwa na wenye mamlaka na kukubalika kuwa zitatangazwa katika mwaka wa fedha ujao. Swali la 9.
Napenda kukipongeza chombo hiki kwa kuwa ninaamini kina fanya kazi kwa uwazi maana suala la ajira ni nyeti lakini nyie mmekuwa mnatoa taarifa za ajira kwenye chombo hiki, tarehe ya kuitwa watu kwenye usaili na pia majina ya walioshinda usaili. Swali langu ni kuhusu tangazo la ajira la March 23 ambalo usaili ulikuwa mwezi Mei kwanini baadhi ya taasisi zimetoa majibu baadhi ya taasisi hazijatoa majibu? Na kama kuna taasisi usaili ulifanyika hakupatikana mtu aliyefaulu usaili huwa inakuwaje? Tunashukuru kwa pongezi zako na kuwa miongozi mwa wadau wengi wanaotambua mchango wa chombo hiki. Inawezekana usipate majibu ya kukuridhisha kutokana na namna ulivyouliza swali lako, kwanza tangazo lililotolewa mwezi Machi ni la tarehe 26 na si 23 kama ulivyoainisha, pili kwa usaili huo unaouelezea jaribu kufafanua ni usaili uliofanywa na Sekretarieti ya Ajira au Taasisi gani ambazo hazijatoa majibu ili tuweze kukufafanualia zaidi. Pili, inapotokea usaili unafanyika na hakupatikana mtu aliyefaulu usaili huo utaratibu wa Sekretarieti ya Ajira ni kutangaza nafasi hiyo kwa mara nyingine (Re-advertisment) Swali 10.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, mimi ni kijana mtanzania mwenye umri wa miaka 31 niliyemaliza masomo yangu nchini Algeria mwezi juni Mwaka 2012 shahada ya Uchumi katika chuo kikuu cha Bejaia nchini Algeria, ambapo muda wa masomo wa shahada hiyo ya uchumi ni miaka 5 yaani mwaka mmoja (1) ni lugha ya kifaransa kama ndo lugha ya kufundishia na miaka minne(4) ndo muda wote wa kusomea shahada! Pia ningependa kutoa maelezo kwamba mimi na watanzania wenzangu (wanafunzi wote wanaosoma nchini Algeria) ni wanafunzi ambao tumepelekwa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kwenda kusoma nchini Algeria kwani huwa inatoa matangazo ya scholarships kwenda kusoma nchi mbalimbali kupitia magazetini na tovuti ya wizara (www.moe.go.tz). Mimi binafsi nilipelekwa na serikali tangu mwaka 2007 mwezi september kupitia wizara iliyokuwa wizara ya sayansi, technolojia na elimu ya juu nikiwa na miaka 25.Vilevile huwa tunahakiki vyeti TCU baada ya kuhitimu. Baada ya maelezo hayo,mimi natambua kwamba ushindani ni mkubwa sana kwenye soko la ajira hasa utumishi wa umma, Lakini je elimu ya Algeria inakidhi vigezo vya kuwa mshindani katika nafasi zinazoombwa? Pia matokeo yetu (Transcripts) hayapo katika mfumo wa GPA maana hata TCU hawaweki GPA zinatambulika? Kama ndio Mimi niliomba nafasi ya kazi katika CHUO CHA NIT na juni 28 2013 wametoa majina MANNE tu ya usaili wa ana kwa ana bila kupita kwenye USAILI WA MCHUJO ili hali mimi pia niliomba kama Records Management officer? Vilevile niliomba TBC kama Marketing Oficer II,ambapo kuna usaili wa mchujo lakini sijaitwa maana kuna watu zaidi ya 60 walioitwa kwenye usaili huo. Ama baada ya hapo, niseme tu nimeendelea kuomba nafasi mbalimbali nyingine katika taasisi yako. USHAURI: mambo mengine ya kuzingatia katika ushindani, Ngarama zilizotumika kumsomesha mwanafunzi mafano mimi nimegharamiwa na serikali kwa gharama na nitaanza kurudisha hizo fedha lini?, umri mkubwa bila uzoefu kazin, lugha zaid ya moja, nafasi ya mtu katika jamii mbali na elimu, usawa wa kijinsia, Makundi maalumu katika jamii(Mfano mimi ni mtu ninayetegemewa sana katika familia ya Mzazi wangu). Tunashukuru kwa maelezo yako, Ni kweli kama ulivyosema fursa za ajira ni chache na waombaji ni wengi hasa katika Utumishi wa Umma, Aidha kusoma nje ya Nchi hakumnyimi mtu fursa ya kuomba kazi katika Utumishi wa Umma Jambo la msingi ni vyeti vyako vya kitaaluma kupata ithibati kutoka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na pia unapoomba nafasi ya kazi unapaswa kwanza kuzingatia masharti ya kila kazi kutokana sifa zilizoainishwa kwenye tangazo husika. Kuhusu kazi ambazo unasema uliomba TBC na NITmchakato wake uliendeshwa na Sekretarieti ya Ajira ila utambue kwamba si kila usaili lazima uanze na hatua ya mchujo. Usaili wa Mchujo unafanyika pale inapotokea waombaji waliokidhi vigezo ni wengi ukilinganisha na nafasi zilizopo lakini inapotokea waombaji ni wachache si lazima kufanya usaili wa mchujo. Pia tunapokea ushauri wako lakini vitu ulivyovitaja si vigezo pekee vya kufanya upate kazi husika bali pia mambo mengine huzingatiwa ikiwemo vigezo vya kitaaluma. Swali la 11
Samahani jina langu limetoka tarehe 18/6/2013 kuwa nimepata kazi barua inayoonyesha kituo gani cha kazi nimepangiwa imeshatumwa kwa Posta lakini cha ajabu ni kwamba nimekuwa nikifuatilia barua hiyo bila mafanikio, je barua hizo zimeshatumwa au bado? ili isije ikaonekana kwamba sijahudhuria kwenye kituo cha kazi nilichopangiwa bila maelezo. Asante, Jibu ni kwamba barua hizo zilishatumwa kwenye anuani ya kila mwombaji aliyefaulu na kupangiwa kituo cha kazi aidha kama hadi kufikia sasa hujapata barua yako ni vyema ukawasiliana na Sekretarieti ya Ajira kwa msaada zaidi. Swali la 12
NATAFUTA KAZI AS COMMUNITY DEVELOPMENT WORKER I am a Tanzanian female age 24 completed Bachelor Degree of Community Development with bias in Gender and Development in CDTI Tengeru Arusha. Kwa kuwa tayari umeshahitimu chuo tunachoweza kukushauri ni kutembelea Tovuti ya Sekretarieti ya ajira www.ajira.go.tz mara kwa mara ambayo ndio hutumika kutoa matangazo ya kazi katika Utumishi wa Umma ili utakapoona kazi ambayo inaendana na taaluma yako uweze kutuma maombi. MWISHO.

Source: http://www.ajira.go.tz/attachments/article/155/HOJA%20II,%20Oktoba.pdf

Microsoft word - single payer is good for business.docx

Published on The Nation (http://www.thenation.com) Single-Payer: Good for Business Morton Mintz | October 28, 2004 Business leaders complain endlessly that the current system of private healthcare insurance based on employment provides fewer and fewer people with less and less quality care at higher and higher cost. Yet Corporate America turns its back on a publicly financed system, whi

Ausgabe märz

Im Frühjahr einmal Tier-Punkt Zum Mitnehmen! mehr zur Bürste greifen Lesen Sie in dieser Ausgabe Afterpartien sollten frei von Haaren sein. Zecken entfernen und richtig „entsorgen“ Über die Ballen und Krallen hinaus soll-ten die Haare an den Pfoten nicht wach- Buchtipp : sen. Zwischen den Ballen dürfen nurVerfilzungen entfernt, aber keine Haare Mit dem Herzen se

© 2010-2017 Pdf Pills Composition